July 25, 2016


Taarifa ni kwamba katika kambi ya Simba huko Morogoro mambo yamenoga katika kampeni na maandalizi ya kurekebisha makosa kwa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao ikiwa chini ya kocha mpya, Mcameroon, Joseph Omog.

Mpaka jana Jumapili, Simba imefikisha wiki mbili ikiwa mkoani humo na sasa imehama kwenye mazoezi ya fiziki na kutengeneza kombinesheni, kilichobaki sasa ni vijana kupambana wenyewe kwa wenyewe kuonyesha ushawishi jinsi gani wameelewa maelekezo ya Omog.

Meneja wa Simba, Abbas Ally, ameeleza kwamba wanashukuru vijana katika kambi hiyo wanaendelea vizuri, hakuna majeruhi wala anayeumwa zaidi ya kunoga kwa mazoezi, wakipambana wenyewe kwa wenyewe katika ushindani wa hali ya juu kila wanapofanya mazoezi ya timu mbili tofauti.

“Maendeleo huku ni mazuri sana tunamshukuru Mungu, wachezaji nao wamesharejea katika ari ya kupambana baada ya kumaliza mazoezi ya kuwarejesha mchezoni baada ya kuwa katika mapumziko ya muda.

“Wachezaji sasa wanapambana kwelikweli, yaani kila mmoja anaonyesha kazi na wanafurahia ushindani uliopo, cha kushukuru ni kwamba hakuna majeruhi wala anayeumwa, ina maana kuwa vijana wapo fiti na wamerejea kazini,” alisema Abbas.

Tayari imeelezwa kuanzia kesho, Simba inaweza kuanza kucheza mechi zake za kirafiki tatu za awali zilizoombwa na Omog kwa ajili ya kuwaangalia vijana wake na kupata tathmini ya kina pia juu ya wachezaji wa nje wanaofanya majaribio kwa sasa kikosini hapo.


Baada ya mchujo kupita, Simba imesaliwa na wachezaji wanne wa majaribio; Wakongo, Janvier Bokungu, Moussa Ndusha, Muivory coast, Blagnon Fredric na Mzimbabwe, Method Mwanjali.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic