July 25, 2016Tayari majina ya waamuzi wa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika wa Yanga dhidi ya Medeama ya Ghana yameshawekwa wazi na kwa mara nyingine baada ya mchezo wa awali wa jijini Dar kuamuliwa na Wamisri, safari hii utaamuliwa na Wamorocco.

Majina hayo yamewekwa juzi na Mtandao wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ambapo mwamuzi wa kati atakuwa RĂ©douane Jiyed akisaidiana na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou.

Jihed mwenye miaka 36, atachezesha mchezo huo mgumu utakaopigwa kesho Jumanne katika Uwanja wa Essipong Sports jijini Sekondi, Ghana ambapo kila timu itahitaji ushindi wake wa kwanza baada ya michezo yao mitatu ya awali kutopata matokeo ya kuridhisha.

Katika mchezo wa awali uliopigwa Dar, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Yanga kubaki mkiani mwa Kundi A baada ya kufungwa katika michezo mingine miwili ya awali. Medeama ipo nafasi ya tatu, imefungwa mechi moja na kutoa sare mbili.


Yanga ina pointi moja, Medeama ina mbili, MO Bejaia ya Algeria inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tano, vinara TP Mazembe ya DR Congo wamekusanya pointi saba mpaka sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV