August 24, 2016


Baada ya kikosi cha Mwadui FC kuchapwa kwa bao 1-0 katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, kocha wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameamka na kusema, anakubali kufungwa lakini akasisitiza, walicheza mechi kwenye uwanja mbovu.

Toto African ndiyo walioichapa Mwadui FC kwa bao 1-0, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Dar es Salaam. Shujaa wa Toto akiwa ni Waziri Junior aliyepachika bao hilo katika kipindi cha kwanza.

“Nakubali kabisa kuwa mchezo nimepoteza kwa kuwa bao lilikuwa hakuna lawama hata  kidogo. Tumepambana mwisho ukashindikana.

“Lakini uwanja tuliochezea, unaweza ni wa kuchezea ng’ombe na si binadamu. Hauna viwango na kweli umeharibika sana.

“Awali tulikuwa tucheze Jumamosi, eti mechi ikaahirishwa kwa kuwa kuna Fiesta na ajabu ligi ilishapangwa, kwa kuwa kuna shughuli ambayo si ya soka, mechi inaahirishwa,” alisema Julio.

Katika mechi hiyo, Mwadui FC walishindwa kung’ara katika kipindi cha kwanza, lakini wakacharuka katika kipindi cha pili lakini hakukuwa na mafanikio.1 COMMENTS:

  1. Saleh jembe hamko serious ccm kirumbo upo dar hahaha hamnifai nyie habar za udaku tu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV