August 28, 2016


Kipa wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ ameisaidia timu yake kuanza vizuri Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon.

Lakini wakati akiwa uwanjani, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, baba yake mzazi aliyekuwa amelazwa amepoteza maisha.

Imeelezwa, kwamba pamoja na Yanga kupata taarifa hizo za msiba, waliona haikuwa sawa kumueleza wakati wa mapumziko, hadi baada ya mechi, alielezwa jambo hilo.

SALEHJEMBE, INAMTAKIA DIDA AWE NA NGUVU, MWENYEZI MUNGU AMUONGEZEE UJASIRI AWEZE KUPITA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MSIBA 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV