August 24, 2016

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa kuwakabidhi kombe jipya la Ngao ya Jamii timu ya Azam kutokana na kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.

Azam waliichapa Yanga kwa penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. 




  Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameliambia Championi Jumatano kuwa, waliwapa Azam ngao ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa kukamilika kwa utengenezwaji wa ngao halali ambalo walitakiwa kupewa.

“Lile kombe ambalo tuliwapa Azam siku ile walipocheza na Yanga kwenye Ngao ya Jamii halikuwa lenyewe, bali tulilitoa kwa ajili ya kuziba nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja kutokana na kutokamilika mpaka inafika siku ile, hivyo tukaona siyo vizuri bingwa akiondoka mikono mitupu.

“Tumepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao halisi ambalo walistahili kupewa ambalo hili litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti kabisa na lile ambalo tulilitoa awali,” alisema Alfred.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic