August 5, 2016


Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Aden Rage, amemtaka Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kumuomba radhi ndani ya siku tatu.

"Nadhani mtu mwendawazimu tu anaweza kufanya hivyo, mke wangu hana hata akaunti. Nimeshamuambia wakili wangu amshughulikie, aniombe radhi ndani ya siku sana. La sivyo suala hili litaenda mahakamani," alisema Rage.

"Sasa hivi tunazungumzia suala la fedha za Okwi na si fedha za Samatta," aliongeza Rage.


Rage amemtaka Hans Poppe kumuomba radhi kutokana na kauli yake kwamba fedha za malipo ya Mbwana Samatta kutoka TP Mazembe, zilipitia kwenye akaunti ya mkewe.


Hans Poppe alisema hayo jana wakati akifafanua kuhusiana na suala lililo Takukuru baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kushikiliwa, kuhojiwa. Baadaye wakahojiwa wajumbe wa kamati ya utendaji.

Rage amezieleza taarifa hizo za Hans Poppe kuwa ni uzushi usiokuwa na maana, hivyo anasisitiza anatoa siku tatu za kuombwa radhi.

1 COMMENTS:

  1. Hamna haja ya kumtaka aombe msamaha kwanza. Huyo peleka kortini moja kwa moja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic