August 7, 2016


Mashabiki wa kikosi cha Simba, wameonyesha kuwa na kiu kubwa ya kuhakikisha kama kweli mshambuliaji Laudit Mavugo ametua nchini na kujiunga na timu yao.

Mashabiki hao walijitokeza kwa wingi kuhakikisha wanamuona Mavugo wakati Simba ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.


Karibu kila shabiki alitaka kumuona au kupiga naye picha na walionekana kufurahishwa na mshambuliaji huyo ambaye amejiunga na Simba akitokea Vital’O ya kwao Burundi.

Meneja wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ alilazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha Mavugo anapanda basi la wachezaji.1 COMMENTS:

  1. mashabiki ni watu wa mihemuko na kuhamasishana kwani sioni rekodi yake kubwa zaidi ya kumsubiri rasmi uwanjani ingawa namsihi ayane maokezi na bashsha kama changamoto kwake

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV