August 7, 2016


Azam FC imeelezwa kuwa moja ya timu zilizofanikiwa kupata majembe hasa kwa ajili ya msimu ujao hasa kwa kumnasa Mzimbabwe, Bruce Kangwa.

Mitandao ya Zimbabwe, imeisifia Azam FC kumpata kiraka huyo kutoka Highlanders kwa kuwa ni mchezaji anayecheza zaidi ya nafasi nne uwanjani tena kwa ushindani wa juu.

Kangwa amejiunga na Azam FC na mitandao ya Zimbabwe inamueleza mmoja wa wachezaji hatari kutokana na kasi na uwezo wake wa kufunga.


Kangwa alikuwa na mabao saba hadi ligi ya Zimbabwe inasimama lakini ameshinda nafasi ya mwanasoka bora kwa miezi mitatu mfululizo.

Pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto, kiungo namba sita lakini kiungo mchezeshaji, wingi wa kushoto au namba kumi na imeelezwa kwamba kila sehemu, anachea kwa ushindani wa juu, hivyo Azam FC haiwezi kupata hasara kwa kuwa ‘ukubwa’ wa msaada wake ni mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV