August 27, 2016


Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, amesema kikosi chake kipo kamili kwa ajili ya mchezo wao wa leo Jumamosi dhidi ya Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, hivyo wapinzani wake hao watamsamehe kwani tayari amewaandalia kipigo.

Simba iliyoanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda, leo itacheza na ‘wajeda’ hao kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Omog amesema lengo lake ni kuona kikosi chake kinashinda katika kila mchezo wa ligi na kukusanya pointi nyingi ambazo zitakuja kuwabeba hapo baadaye katika kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

“Tunataka kuwa mabingwa, kila siku nasema hivi na watu wamekuwa kama hawaamini, ili kudhihirisha hilo, tumeanza kwa ushindi kwenye mchezo wa kwanza, tunaenda tena mchezo wa pili kushinda.

“Huwezi kuwa bingwa bila ya kushinda mechi nyingi, tumedhamiria kupata pointi tatu kwenye kila mchezo wetu, hivyo JKT Ruvu watatusamehe tu kwani lazima tuwafunge.

Najua na wao wamejiandaa kama sisi, lakini hilo halituzuii kushindwa kuwafunga kwa sababu tuna kikosi imara na wachezaji wenye uwezo kuliko wao,” alisema Omog.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic