August 6, 2016

MAGURI AKISHANGILIA BAADA YA KUFUNGA BAO.

Mshambuliaji Mtanzania, Elius Maguri ameanza kuonyesha cheche zake nchini Oman.

Maguri ameifungia timu yake ya Dhofar SC ya nchini Oman bao moja wakati ikishinda 2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Al Etihad.

Al Etihad inashiriki daraja la kwanza ikiwa inapambana kupanda Ligi Kuu nchini Oman.


Maguri alifunga bao la kwanza katika mchezo huo ambao ni sehemu ya yeye kuanza kuzoea mazingira ya kisoka ya Oman.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV