August 17, 2016

Manchester City imeanza vizuri kampeni zake za kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutoa kipigo kikali kwa Steaua Bucharest cha mabao 5-0 licha ya kuwa matajiri hao wa Jiji la Manchester walikuwa ugenini.
   
Aguero akipunga mkono baada ya kutupia wavuni.

Kipa wa Man City, Caballero akipongezana na kiungo wake Fernandinho mara baada ya mchezo huo.


Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na Man City kwa asilimia kubwa Kocha Pep Guardiola alionekana kuw ana kazi nyepesi ya kuwapa maelekezo wachezaji wake kwa kuwa upinzani ulikuwa ni wa kiwango cha chini kiasi kwamba City ni kama walikuwa mazoezini.

Ndani ya kipute hicho ambacho ilishuhudiwa kipa namba moja wa Man City, Joe Hart akiendelea kusugua benchi, straika Sergio Kun Aguero alifunga mabao matatu huku akikosa penalti pia.

Aguero alifunga mabao hati katika dakika ya 41, 78 na 89, wakati ambapo mabao mengine yaliwekwa wavuni na David Silva dakika ya 12 na Nolito dakika ya 49.

Timu hizo zitarudiana Agosti 24, mwaka huu na baada ya hapo itafuata hatua ya makundi rasmi.

Matokeo mengine ya mechi hizo za kuania kufuzu hatua ya makundi yalikuwa hivi:

Ajax 1 – 1 FC Rostov
Dinamo Zagreb 1 – 1 Salzburg
FC Koebenhavn 1 – 0 APOEL Nicosia
Young Boys 1 – 3 Borussia Moenchengladbach


Guardiola akitoa maelekezo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV