Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kiungo wake kinda, Juma Mahadhi ataendelea kufanya kweli kama akiwa makini katika nidhamu, pia kujituma.
Pluijm amesema Mahadhi ana bahati kwa kuwa ana kipaji ambacho kinatakiwa kuendelezwa.
Yanga imeanza Ligi Kuu Bara kwa kuitandika African Lyon kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo, Mahadhi alifunga bao la tatu, muda mchache baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Kaseke.
Alifunga bao hilo safi kwa shuti kali nje ya eneo la 18 la African Lyon.
0 COMMENTS:
Post a Comment