August 10, 2016

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI.
Kutokana na sababu mbalimbali, Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imelazimika kubadili Ratiba ya Ligi Kuu kwa michezo kadhaa ya mwanzo kama ifuatavyo.

1. Mchezo Na. 2 - Kagera Sugar vs Mbeya City (20.08.2016)

Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 21.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Sababu ni kuwa uwanja wa Kaitaba bado utakuwa kwenye matengenezo.
 2. Mchezo Na.4 - Toto African vs Mwadui FC (20.08.2016)

Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 24.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kirumba. Sababu za mabadiliko ni kuwa uwanja huo tarehe 20.08.2016 utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.
3. Mchezo Na.13 - Kagera Sugar vs Stand United (27.08.2016)

Mchezo huo sasa utachezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage. Awali timu mwenyeji wa mchezo huo ilikuwa ni Kagera Sugar, lakini kwa sasa timu mwenyeji atakuwa ni Stand United.
4. Mchezo Na.55 - Toto vs Ndanda (02.10.2016)

Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 03.10.2016 badala ya tarehe 02.10.2016
5. Mchezo Na.80 - Mbao FC vs Ndanda fc (16.10.2016)

Mchezo huo umerudishwa nyuma kutoka tarehe 16.10.2016 hadi tarehe 28.09.2016. Sababu ni kuiwezesha timu ya Ndanda kucheza michezo miwili kwa kanda ya ziwa kwa lengo la kupunguza gharama.
6. Mchezo Na.96 - Tanzania Prisons vs Mbao FC (22.10.2016)



Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 23.10.2016 badala ya 22.10.2016 ili kuipa nafasi timu ya Mbao kupumzika na kusafiri. Tayari timu za Ligi Kuu ya Vodacom zimearifiwa na kuagizwa kuzingatia mabadiliko hayo.

2 COMMENTS:

  1. Mara nyingine si haki kuilaumu TFF,TFF haimiliki viwanja,wao ni wapangaji wa ratiba tu,kuendelea kuilaumu TFF ambayo haina mamlaka na viwanja ni uonevu wa bure.

    Suruhisho la pekee la panga pangua hii ya ratiba ni vilabu vyenyewe kumiliki viwanja vyao badala ya kuendelea kutumia viwanja vinavyoitwa vya ccm.Wamiliki wanaweza kuvihitaji muda wowote kwa matumizi yao na TFF isiwe na uwezo wa kuwazuia.

    FIFA inahimiza clabu kuwa na viwanja vyao kwa ajili ya kuepuka mambo ya namna hii.

    ReplyDelete
    Replies
    1. safi sana umejibu vyema uandishi uchwara wa namna hii

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic