January 18, 2021


 ANAITWA Junior Lukosa raia wa Nigeria anatajwa kuingia kwenye rada za Simba kwa ajili ya michuano ya kimataifa kwa kuwa Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya makundi.


Licha ya dirisha la usajili wa Bongo kufungwa Januari 16 bado Simba ina nafasi za kusajili kwa mujibu wa Caf ila wachezaji hawa watatumika kwenye Ligi ya Mabingwa pekee.

Junior ana uzoefu wa kucheza soka la Afrika ikiwa amecheza ndani ya Klabu ya Esperance ya Tunis, Kano Pillars ya Nigeria na alikuwa anacheka na nyavu tu.

Ana umri wa miaka 27 ana uwezo wa kucheka na nyavu ambapo akiwa na First Bank pia alikuwa anafunga kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Akiwa na Pillars aliweza kutupia jumla ya mabao 19 ilikuwa msimu wa 2018/19 na ana tuzo ya mfungaji bora baada ya kucheza zaidi ya mechi 20.

Ndani ya Klabu ya Esperance ya Tunis alipata nafasi ya kucheza mechi 11 za mashindano sita na Ligi ya Mabingwa Afrika alicheza mechi nne.

Inaelezwa kuwa Klabu ya Simba inahitaji saini ya nyota huyo ili aweze kuongeza nguvu kwa kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola.

13 COMMENTS:

  1. Mwandishi hujui hata kupangilia taarifa, hujui kitu gani cha kuandika ili habari yako iwe na mashiko. Unaandika andika ilimradi umeandika. Unachoangalia ni kupamba tu kichwa cha habari ili kuvutia wasomaji lakini main body ya habari yenyewe ni hovyo kabisa

    ReplyDelete
  2. Hao ndio wachezaji wa kusajili hata akipatikana mchezaji kinda mahiri mwenye uwezo wa kuogonga mwingi kimataifa simba wasajili kwa kulenga biashara pia.Wakati mwengine timu kubwa za kiafrica hazina wakati za kuchungulia vipaji vipo wapi wanasubiri kutafutiwa watumie pesa zao.viongozi wetu wa simba wafikirie hilo la biashara pia kwenye hizi nafasi 10 za ziada za Caf. Wanaweza kuskauti makinda ya kawaida yenye viipaji visivyo vya kawaida kwa ajili ya showing case kwenye hatua ya makundi kwa minajili ya biashara. Simba ipo kwenye opportunity kubwa kabisa baada ya kukolifai hatua ya makundi wanasimba na watanzania tunapaswa kujivunia na kutembea kifua mbele na mazuri mengi yana kuja tuwe na subira.

    ReplyDelete
  3. Kama kweli kwanini msingemalizana naye mapema

    ReplyDelete
  4. upuuzi tu we mwandishi hujui hata kupangilia habari

    ReplyDelete
  5. Makundi,Lakini round ya pili zingatia Hilo but no mafanikio mazuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwan baada ya hapo kuna makundi tena.... Au we ni UTO

      Delete
    2. Huyu jamaa anayejiita rogatus anang'ang'ania Simba ipo hatua ya pili Yani anaonekana mpira hajui lkn Kila siku lazima achangie nada zinazoihusu Simba jamani Kama mmekuwa washabiki wa Mpira kupitia YouTube sio lazima mchangie unatumia nguvu kubwa toka juzi kuwaaminisha watu kuwa Simba haijafanya chochote Cha maana tuambie wewe utopolo Mara ya mwisho kuingia hatua ya makundi ligi ya mabingwa ilikuwa mwaka gani,miaka 3 yote Kila mkiingia mnatolewa mnaishia kuwa best looser,eti makundi lkn round ya pili Yani inadhiirisha kuwa wewe kweli ni tahira Bora ukae kimya

      Delete
    3. Huyo sijui rogatus Haina haja anaonekana hata anachochangia hakiju eti makundi lkn round ya pili,Sasa round ya pili nayo tutaiitaje,alafu anasema no mafanikio kuingia robo fainali kwenye lenye timu Kama Ahly , AS Vita,JS soura sio mafanikio ama kweli utopolo wanateseka kwa kuwa wanajua wao kuja kufika hatua hizo Wana Safari ndefu sana,kwa hiyo wanataka kuwaaminisha watu kuwa ni rahisi tu kuingia hatua ya makundi ligi ya mabingwa jitu ambacho wakishinda kufanya kipindi Cha Manji kwa miaka 4,alafu Simba ndani ya miaka 3 imeingia Mara 2 mtateseka sana WEHU nyinyi

      Delete
    4. Ni vizuri wasiojua wakajua kuwa Simba imeingia kumi na sita(16) bora Club bingwa Afrika.Kwa kweli siyo hatua ya kubeza. Ni heshima kubwa kwa Taifa. Tukiingia hatua ya robo fainali tutafurahi zaidi ila ikatokea baati mbaya tukashindwa kusonga tuna jambo la kujivunia
      .

      Delete
  6. Waandishi wengi hawajui ni vitu gani muhimu vya kuhusisha kwenye habari zao

    ReplyDelete
  7. Naomba niulize kwa hiyo wachezaji hawa 2 ni kwa ajili ya ligi ya mabingwa pekee? Na tukitolewa hawata cheza ligi? Naomba nijuwe hilo nduguzangu

    ReplyDelete
  8. Hehehe... mikia aka paka mweusi mbona mnaweweseka? Acha tusubiri yajayo...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic