August 16, 2016

Taarifa za Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kudaiwa kujiuzulu nafasi yake hiyo, mwanachama mkongwe wa klabu hiyo, Ibrahim Omary Akilimali maarufu kwa jina la Mzee Akilimali ameibuka na kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo kuomba radhi kwa kauli zake.

Wakati huu ambapo Manji hatatoa tamko lolote juu ya uamuzi wake huo wa kujiuzulu, Mzee Akilimali kwanza alinukuliwa akisema kuna watu wa Yanga wamemuita ili kuzungumza kuumaliza mvutano unaoendelea ambapo inaelezwa kuwa mzee huyo amechangia maamuzi ya Manji kujiondoa Yanga kutokana na kumshutumu kwa maneno mengi.



Mzee Akilimali alipokuwa na mazungumzo na Manji siku za nyuma.

Awali alisema “Msitake kuyakuza haya mambo, subirini kwanza nataka tuyamalize, mimi wameniita ndiyo maana nipo huku ili kuyamaliza.”

Alipoulizwa yupo wapi na ameitwa na nani, Akilimali alizema: “Nimekwambia nimeitwa huku, wewe subiri kwanza tuyamalize kisha utanipigia, subiri baada ya nusu saa nitakubeep unipigie.”

Baadaye alipopigiwa simu mzee huyo alisikika kama mtu ambaye amepoa na kuwa mpole ambapo alisema anawaomba radhi Wanayanga kama atakuwa amewakosea kwa kauli zake lakini nia yake ni kuitaka Yanga iwe moja na Manji aonyeshe heshima kwa wazee wa klabu hiyo.


  “Manji ni kijana wetu, sisi wazee nikiwemo mimi tulichangia yeye kuingia ndani ya Yanga, hata mimi ndiye niliyemkabidhi ngao ya uchifu wa Yanga, sasa hapo katikati alikuwa hatushirikishi sisi wazee kama ilivyokuwa zamani.

“Akawa anafanya maamuzi anayoyajua yeye, nia yetu sisi wazee ni kuifanya Yanga iwe moja kuwe na mshikamano, unajua Manji ametutoa mbali, sisi ni Yanga moja, kwa mapenzi yangu yote nataka Yanga iwe kitu kimoja. Yanga ni moja na hakuna mpasuko.



1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic