August 29, 2016Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao, aliyesifiwa kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha walipoumana na Simba na kupata sare ya 0-0 wikiendi iliyopita, ameeleza wazi kilichowaangusha Wekundu hao siku hiyo kuwa ni kukosa mastraika wazuri.

Kauli hiyo ni kama kuwakejeli mastraika wa Simba waliosajiliwa kwa mbwembwe nyingi; Mrundi Laudit Mavugo na Muivory Coast, Fredric Blagnon waliocheza mechi hiyo na kushindwa kufurukuta.

 Licha ya uwepo wa mastraika wa kutumainiwa hao wa kutumainiwa pamoja na Ibrahim Ajib na wengine wengi, kipa huyo alisema hawakuwa na jipya la kuizidi ujanja ngome ya timu hiyo.

“Kiukweli nilijipanga kwa ajili ya mechi, shida kubwa ni kupigania timu yangu isifungwe na imewezekana, ingawa hata hawa mastraika wa Simba nao hawakuwa na ujanja wa kunifunga, hawako makini katika kulenga upande wafunge.

“Namaanisha hata huyo Mavugo hana uwezo mkubwa wa kufunga, walishindwa kuilaghai ngome yetu ya ulinzi lakini waliponifikia pia walishindwa kufanya lolote. Hii itakuwa mpaka tutakapocheza na Yanga Jumatano, tumepania kuondoka na pointi tatu, kwa hiyo hata kina Ngoma (Donald) na Tambwe (Amissi) wajipange,” alisema Kipao.


Katika mchezo huo, kipa huyo alifanikiwa kuokoa mipira ya hatari 16 kati ya mara 17 ambayo Simba ilipenya na kuingia kwenye 18 ya JKT kujaribu kufanya majaribio ya kufunga bao.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV