August 30, 2016

MASAU

Ruvu Shooting wanajua kwamba wanakutana na Simba katika mechi mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara.

Hivyo wameamua kufanya ujanja huu, wamepumzisha wachezaji wapatao wanane ili waisubiri Simba katika mechi hiyo itakayopigwa kesho Jumatano ijayo.

Wakati kikosi cha Shooting kinaondoka Ruvu mkoani Pwani kwenda Songea kuwavaa Majimaji, wachezaji hao waliendelea na mazoezini.

“Kweli wachezaji kama wanane hivi wakiwemo wale wapya kama Fullzuri Maganga na wenzake wamebaki kambini.

“Walikuwa kwenye michuano ya majeshi, lakini sasa wanajiandaa kwa Simba wakati sisi tunatoka Songea, tunaungana nao.


“Ninaamini kabisa hawa Simba tutawafunga. Tuna kikosi bora kabisa. Nilianza kusema kuhusiana na Mtibwa, watu wakadharau, lakini waliona,” alisema Masau.

Katika mechi iliyopita, Simba ilibanwa na Ruvu JKT na kutoka nayo sare ya bila kufungana. Hivyo itakuwa na hasira ya kutaka kubadili gia mbele ya mashabiki wake kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV