Mkongwe Mussa Hassan Mgosi, binafsi alikubali kutoingia kwenye usajili wa Simba ili aanze kufanya kazi za kiungozi.
Mgosi hayumo kwenye usajili wa Simba baada ya viongozi kukaa na kuzungumza naye.
“Unajua msimu uliopita ndani ya kikosi kulikuwa na hali ya kutoelewana, lakini Mgosi alikuwa kama kiongozi na kuweka mambo mengi vizuri.
“Kutokana na hali hiyo, uongozi ulimuomba nafasi yake asajiliwe mchezaji mwingine na yeye aendelee kuwa kama sehemu ya uongozi katika benchi la ufundi, akakubali,” kilieleza chanzo.
Mgosi ni kati ya wachezaji wa Simba na imeelezwa yuko njiani kuanza kozi za ukocha ili baadaye aingie katika taaluma hiyo.
Wanasimba watamkosa katika kikosi cha Simba msimu ujao kutokana na kutojumuishwa na sasa atakuwa sehemu ya benchi la ufundi.
Uongozi wa Simba uliona unamhitaji lakini kasi yake na msaada katika kikosi si mkubwa hivyo kuamua kuzungumza naye.
0 COMMENTS:
Post a Comment