September 18, 2016

Dili la mshambuliaji Emmanuel Adebayor kujiunga na timu ya Lyon ya Ufaransa limekwama na klabu hiyo imetoa taarifa rasmi ya kusitisha mchakato wa mazungumzo ya usajili.


Adebayor ambaye mara ya mwisho alikuwa akiichezea Crystal Palace ataendelea kutokuwa na klabu kwa kuwa alikuwa asajiliwe akiwa mchezaji huru. Hivyo hili sasa ni pigo lingine kwa kuwa katika dirisha la usajili lililopita pia hakuna klabu iliyofikia makubaliano naye katika usajili.


Adebayor alikutana na Kocha wa Lyon, Bruno Genesio, juzi Ijumaa lakini baada ya mazungumzo ilionekana kuwa hawakukubaliana vitu huku klabu hiyo ikionekana kutokuwa tayari kumkosa kwa muda wa mwezi au zaidi kwa kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kushiriki katika michuano ya Afrika akiwa na timu yake ya taifa ya Togo.

Nafasi hiyo aliyotakiwa apewe Adebayor sasa imeenda kwa chipukizi mwenye umri wa miaka 19, Jean-Philippe Mateta ambaye amesajiliwa akitokea ligi ya daraja la tatu.

Lyon ilihitaji straika mmoja kutokana na Alexandre Lacazette kuwa majeruhi.


Michuano ya Afrika inatarajiwa kucheza nchini Gabon, mwakani kuanzia Januari 14 hadi Februari 5.

KLABU ALIZOCHEZA ADEBAYOR
2001–2003 - Metz
2003–2006 - Monaco
2006–2009 - Arsenal
2009–2012 - Manchester City
2011 - Real Madrid (mkopo)
2011–2012 - Tottenham Hotspur (mkopo)
2012–2015 - Tottenham Hotspur
2016 - Crystal Palace

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV