September 18, 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ametoa ofa kwa wananchi kujumuika pamoja leo Septemba 18, 2016 katika mchezo wa mpira wa miguu utakaozikutanisha timu za vijana taifa za Tanzania na Congo-Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zitakutana kweye mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka. Zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itafayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo.
 

Nape alitoa ofa hiyo tangu jana Septemba 17, 2016 na leo asubuhi Septemba alipata kifungua kinywa na wachezaji wa Serengeti Boys ambako alitoa Sh 200,000 kwa kila mchezaji zilizotokana na kundi linalosapoti Serengeti Boys ambao walichangia Sh 2,600,000 wakati nyingine zilitoka kwa wadau wengine.
Serengeti Boys

Nape ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake itakuwa Sh 5,000,000. “Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa fedha zaidi, kwa hiyo Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo mbele ya Watanzania watakaoingia uwanjani bure.”

Kuingia bure kesho ni ofa iliyotolewa na Nape ambako Rais Jamal Malinzi amemshukuru Nnauye ambaye ni Mbunge wa Mtama kwa ofa hiyo ambayo imelenga kutoa hamasa kwa Watanzania kwenda kushangilia timu yao.

Waziri Nape

Katika mchezo huo ambao Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, amesema kwamba amemaliza kila kitu na kwamba anasubiri Watanzania kuja uwanjani leo kuishangilia timu yao, utachezwa na waamuzi kutoka Shelisheli ambako mpiga kipenga atakuwa Nelson Fred akisaidiwa na Hensley Petrousse na Stive Marie wakati mwamuzi wa akiba akiwa Allister Barra. Kamishna wa mchezo atakuwa Gladmore Muzambi kutoka  Zimbawe.

2 COMMENTS:

  1. Mchezo unaanza saa ngapi.mara tunasikia saa 9 mara saa kumi hatuelewi

    ReplyDelete
  2. Mchezo unaanza saa ngapi.mara tunasikia saa 9 mara saa kumi hatuelewi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic