September 3, 2016Kagera Sugar imeichapa Mwadui FC kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Baada ya kipigo hicho, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametangaza kustaafu ukocha akisema huu ndiyo msimu wake wa mwisho.

Julio ameilalamikia Kagera Sugar ambayo iko chini cha Chama cha Soka Mkoa wa Kagera, Jamali Malinzi ambaye ndiye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Kila mtu ameona hakukuwa na hakika, kweli nitaachana na mpira nifanye vitu vingine. Kama ni kufundisha, basi bora nifundishe nje ya Tanzania,” alisema Julio akionekana kuwa na hasira.


Julio alilalamika kwamba waamuzi walifanya matendo ambayo yalionyesha wazi kuwa walitaka lazima Kagera iibuke na ushindi.

2 COMMENTS:

  1. Aaache uzushi gem walicheza vzr kipindi cha kwnza kikwazo kikawa Husen Sharifu kipa wa Kagera,kipindi cha pili Kagera wakacheza mpira na kupata bao ambalo ni uzembe wa Kado.Hakukuwa na upendeleo wowote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo mzee was kubwatabwata turn hana jipya. Hakuna mechi anafungwa kihalali. Kila siku kuna njama dhidi yake. Akajaribu bahati yake nje ya nchi lakini lugha ianze kupanda

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV