September 3, 2016

IHEANACHO
Taifa Stars imemaliza mechi ya mwisho ya kundi lake kuwania kucheza Kombe la Dunia kwa kupigwa bao 1-0 dhidi ya Nigeria.

Kelechi Iheanacho anyekipiga Manchester City alifanikiwa kufunga bao hilo dakika ya 78 kwa shuti kali nje ya 18, hata hivyo, hiyo haikumzuia kipa Aishi Manula kuibuka na kuwa mchezaji bora wa mchezo.

Mechi hiyo Stars ikiwa ugenini, ilicheza vizuri na kushambulia vizuri lakini haikuwa makini katika umaliziaji.


Hata hivyo, Nigeria ndiyo walioshambulia sana na washambuliaji wake hasa Victor Moses na Alex Iwobi walipoteza nafasi nyingi zaidi za kufunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV