September 7, 2016Baada ya kufanikiwa kuongoza Ligi Kuu Bara hivi karibuni, Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema anajipanga vilivyo kuhakikisha timu hiyo haishuki katika nafasi hiyo.
Mbeya City kwa sasa inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi saba ilizojikusanyia baada ya kushuka uwanjani mara tatu huku ikishinda mechi mbili na kutoka sare moja.

Phiri amesema hivi sasa yupo katika mikakati kabambe itakayoiwezesha timu hiyo kuhakikisha haishuki kutoka katika nafasi hiyo kwa sababu safari hii anataka aandike historia mpya hapa nchini.

“Tunamshukuru Mungu kwa nafasi hii tuliyopo hivi sasa kwani ni mwanzo mzuri kwetu katika kuhakikisha safari hii tunafanya vizuri katika michuano hii licha ya ushindani kuonekana kuwa mkubwa sana.

“Hata hivyo, hivi sasa nipo katika mikakati kabambe ya kuhakikisha hatushuki katika nafasi hiyo kirahisi badala yake tunataka kuendelea kuongoza ligi,” alisema Phiri.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV