September 7, 2016Beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amekubali kwa roho moja kuwa sasa si rahisi tena kurejea moja kwa moja na kuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na sababu.

Cannavaro ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu na kukosa baadhi ya mechi za michuano ya kimataifa pamoja na mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya African Lyon, alisema moja ya sababu ya kutoa kauli hiyo ni usajili wa wachezaji wapya kikosini unaomjumuhisha Andrew Vincent ‘Dante’.

“Kila kitu kina mwisho wake kaka, huwezi kuwa kwenye kikosi cha kwanza kwa misimu yote. Kwanza haya majeraha yamenisumbua sana halafu pia kuna watu wapya sasa hivi ambao nao wanatekeleza majukumu vizuri tu.

“Kuna Dante, Bossou (Vincent) wanafanya kazi nzuri. Watu walituzoea nikiwa na Yondani (Kelvin) lakini sasa hivi tukiwa hatupo bado kazi inafanyika vizuri kwa hiyo sasa hakutakuwa na tegemeo kwamba lazima fulani na fulani wawepo, halitakuwa tena suala la mazoea tutakuwa tunapokezana kwa ajili ya timu maana wote tuna uwezo mzuri,” alisema Cannavaro.


Cannavaro ambaye ana umri wa miaka 34 sasa, alianza kuaminiwa katika majukumu ya kikosi cha kwanza cha Yanga tangu msimu wa 2007-08 na alikabidhiwa kitambaa cha unahodha msimu wa 2013-14, baada ya kustaafu kwa nahodha wa awali, Shadrack Nsajigwa.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV