September 4, 2016Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil ameweka wazi kwamba anaitaka jezi namba 10.

Jezi hiyo imeachwa na kiungo Jack Wilshere ambaye ameondoka Arsenal na kujiunga na Bournemouth.

Ozil amesema kama iko huru, basi anahitaji kuichukua jezi hiyo ambayo aliitumia kabla ya kujiunga na Arsenal.

Hivi karibuni, baada ya mshambuliaji Lukas Podolski kutangaza kustaafu katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani, Ozil pia aliomba kupewa jezi namba 10 alikuwa akiitumia.


Kwa sasa kwenye kikosi cha Arsenal, Ozil amekuwa akitumia jezi namba 11 lakini katika kikosi cha Ujerumani anatumia namba 8.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV