September 9, 2016

Baada ya Simba kuibuka na ushindi wa pili katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara, vigogo wa timu hiyo wameamua kuwamwagia noti wachezaji hao ikiwa kama pongezi ya ushindi wao huo. 



Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo huo uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar lakini dakika chache baada ya kumalizika kwa mchezo huo, wachezaji hao wakapewa zawadi hiyo ya kitita cha shilingi milioni tano. 

 
Mmoja wa watu wa ndani wa timu hiyo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, fedha hizo walitengewa tangu walipocheza mechi yao ya pili ya ligi dhidi ya JKT Ruvu, lakini kwa kuwa hawakuibuka na ushindi, hawakupewa chochote mpaka walipoifunga Ruvu.

“Hizo fedha zilikuwepo tangu awali, wenyewe tu kwa kuwa hawakufanya vizuri katika mechi na JKT ndiyo maana hawakuambulia kitu lakini imekuwa safi wameshinda katika mchezo na Ruvu Shooting, ndiyo maana wamepewa zawadi yao na itagawanywa kulingana na mchango wa kila mchezaji, aliyeanza ‘first eleven’, aliyekaa benchi mpaka jukwaani,” alisema kigogo huyo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic