September 13, 2016

Licha ya awali Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kudai kuwa straika Zlatan Ibrahimovic anaweza kuwa na maisha magumu ya uwanjani katika Premier League baada ya kutu Manchester United msimu huu, kocha huyo ameonyesha dalili za kubadili kauli yake hiyo.

Wenger ambaye leo timu yake itakuwa uwanjani kucheza dhidi ya timu ya zamani ya Zlatan, Paris Saint-Germain ya Ufaransa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, amesema kuwa Ibrahimovic ni mchezaji muhumu na PSG imepata pigo kumpoteza.


Zlatan akiwa Man United.

Zlatan alipokuwa PSG

Wenger

  PSG leo itakipiga dhidi ya Arsenal ikiwa inawategemea Edinson Cavani na Jese Rodriguez kwenye safu ya usambuliaji, ambapo Wenger anaamini PSG itakuwa na wakati mgumu.

“Alikuwa kiongozi, nahodha na mwenye wasifu mkubwa kuiongoza timu, ukimpoteza mchezaji wa aina hiyo ni pigo,” alisema Wenger.

Tangu atue ndani ya Man United mpaka sasa amefunga mabao manne katika michezo minne ya Premier League aliocheza.

PSG imeshindwa kupata ushindi katika mechi zake mbili zilizopita na inaonekana inapata wakati mgumu kuzoea mazingira ya kucheza bila Zlatan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV