September 12, 2016

 Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametimiza ahadi yake yake ya kumpa zawadi ya gari beki Mohamed Hussein Zimbwe.

Blog hii ilikuwa ya kwanza kuandika kuhusiana na uamuzi huo wa Hans Poppe.

Hans Poppe aliahidi hivyo msimu uliopita kwa Zimbwe Jr na mshambuliaji Hamisi Kiiza ambaye hata hivyo, baadaye alieleza wazi kuwa ‘anazingua’ na asingefanya hivyo.

Hans Poppe ambaye ni muwazi, alisisitiza lazima angempatia zawadi hiyo Zimbwe.

“Zawadi ya gari hii hapa kwa mchezaji anayejituma na kutambua wajibu wake,” alisema.Amemkabidhi gari aina ya Toyota Raum ambalo Hans Poppe amesema beki huyo kinda, alichagua mwenyewe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV