September 12, 2016

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anapata wakati mgumu kwa kuwa kuna uwezekano wa kumkosa nahodha wake, John Terry kuelekea katika mchezo dhidi ya Liverpool katika Stamford Bridge, Ijumaa ya wiki hii.

Terry alipata majeraha ya mguu na kuna uwezekano wa kuukosa mchezo huo, ikiwa itakuwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa beki David Luiz kupata nafasi kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa hivi karibuni akitokea PSG.
 
Terry alitoka kwenye Uwanja wa Liberty akichechemea katika mchezo wa jana ambapo timu yake ilipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea City.

Baadaye mchezaji huyo alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha mguu wake ulivyokuwa ukiopatiwa matibabu na madaktari wa klabu yake.

Akimzungumzia Terry, Conte alisema: "Sijui ukubwa wa jeraha, kesho tutafahamishwa kuhusu maumivu yake ya mguu ila sina hofu kubwa sana."

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV