September 12, 2016

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes amewakosoa mabeki wa timu hiyo, Daley Blind na Antonio Valencia kwa jili walivyocheza katika mchezo wa Manchester derby dhidi ya Manchester City.

Scholes amenukuliwa akisema: “Blind ni zuri akichea kama kiungo mkabaji na siyo beki wa kati, japokuwa hivi karibuni amekuwa akielewana na Eric Bailly.

“Nashindwa kuelewa kwa nini Chris Smalling hachezi.


Scholes“Kwa nini nasema Blind ni tatizo pale, kwanza hana nguvu sana wakati katika Premier League hilo ni jambo la muhimu katika mechi dhidi ya City alishindwa kuwa mwpesi kuendana na Kevin de Bruyne.

“Ningependelea kumuona Smalling akicheza pamoja na Bailly.”

Kuhusu Valencia, mkongwe huyo alisema: “Valencia siyo beki wa kulia na hatakuwa kamwe, Matteo Darmian hajapata kasi ya kuendana na ligi na ninachojiuliza kama Timothy Fosu-Mensah anaweza kuanza katika kikosi cha kwanza au la, nafikiri kuan tatizo hapo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV