September 4, 2016


Lile shauri la malalamiko ya klabu ya Simba kuhusiana na beki hassan Kessy liliahirishwa, lakini kuna kila dalili linaweza kusikilizwa upande mmoja na kutolewa maamuzi.

Hali hiyo inatokana na Yanga kutohudhuria katika kikao cha kwanza na hadi linaahirishwa kutosikilizwa leo, hawakuwa wamesema chochote.

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iimeahirisha kikao chake kilichokuwa kikae leo Jumapili Septemba 4, 2016 kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na klabu ya Young Africans sambamba na kusajili katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho Juni 15, 2016.

Kamati hiyo imesema itaandika barua kuwakumbusha Yanga kuhusiana na kuhudhuria, kama wakishindwa basi litasikilizwa upande mmoja na kutokewa maamuzi.

"Shauri la Simba dhidi ya Young Africans lilishindika kusikilizwa kwa sababu Young Africans hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo, hivyo kamati itaiandikia barua Young Africans kukumbushwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo Jumapili ijayo kabla ya kutolewa uamuzi.

"Kama hawakutokea tena, shauri hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja. Kadhalika mashauri mengine yatakayosikilizwa hapo baadaye ni pamoja na yale ambayo wahusika walipewa nafasi ya kuyamaliza nje ya kamati lakini wakashindwa," ilieleza sehemu ya taarifa ya TFF.

Simba wanalalamika kuwa Kessy aliingia mkataba na Yanga kabla ya kumaliza ule wa kwake na Simba.

Lakini tayari TFF imemruhusu kuendelea kucheza, jambo ambalo Simba pia wanalipinga huku wakisisitiza kulipwa zaidi ya Sh bilioni 1 ambazo ni sehemu ya uvunjwaji wa mkataba kwa kuwa kipengele hicho kipo kwenye mkataba wao na Kessy.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic