September 4, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema wanachotakiwa ni ushindi kwa mechi zaidi ya mbili zijazo ili kujiweka sawa kwamba sasa wamerejea kwenye ligi.

Pluijm raia wa Uholanzi amesema ushindi wa mechi moja, hauwatoshi ni lazima washinde ili kuinua morali na kuweka hisia wako wapi.

“Lazima turudishe morali miongoni mwetu, tunatakiwa kuhakikisha tunashinda mfululizo halafu tutajiweka sawa,” alisema.

“Tunajua ligi itakuwa ngumu, lakini nguvu ya ushindi itaongezeka kila tunaposhinda na kuinua morali.”


Yanga inaingia kambini kesho tayari kwa maandalizi ya mwisho dhidi ya Ndanda FC katika mechi yake ya pili ya ligi baada ya kuanza kwa kuichapa African Lyon kwa mabao 3-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV