September 19, 2016

Kuondoka kwa beki Dan Alves katika kikosi cha Barcelona bado ni pigo na ndiyo maana klabu hiyo imekuwa ikiendelea mchakato wa kutafura mchezaji sahihi anayeweza kuziba nafasi hiyo.

Beki wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin ametajwa kuwa ndiye anayongoza katika listi ya Barcelona katika dadi ya wachezaji wanaotakiwa kikosini hapo.

Hector Bellerin (kulia)

Mchezaji huyo amekuwa akifanya vizuri chini ya Kocha Arsene Wenger na hiyo ni moja ya sababu ambayo imemfanya Kocha wa Barcelona, Luis Enrique kuhitaji kumsajili.

Bellerin ambaye ana umri wa miaka 21 alizaliwa Barcelona na akaanza maosha yake ya soka akiwa na klabu hiyo kabla ya baadaye kuondoka akiwa katika kituo cha La Masia mwaka 2011, hivyo Barcelona wanataka kumrejesha nyumbani kijana wao kama ilivyokuwa kwa Cesc Fabregas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV