September 13, 2016

Klopp
 Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametoa amri ya jambo moja kufanyika ambalo limeenda kinyume na utaratibu wa klabu yake hiyo ambayo ni maaarufu kwa kuvaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe.

Klopp ameagiza nyavu za Uwanja wa Anfield unaomilikiwa na klabu hiyo zibadilishwe rangi kuwa nyeupe badala ya nyekundu kama zilivyokuwa awali.

Liverpool iliamua kuweka rangi nyekundu katika nyavu za magoli yake uwanjani hapo ikiwa ni ishara ya kuendeleza kile ambacho wao wanaamini ni utamaduni wa rangi nyekundu za klabu hiyo, jambo ambalo limepingwa vikali na Klopp ambaye ana umri wa miaka 49.
 

Sababu za Klopp kukataa rangi nyekundu katika nyavu hizo na kuwa kuwa hazina muonekano mzuri kwa wachezaji wake ambao nao wanvaa jezi nyekundu wakiwa uwanjani hapo.

Ametaka ziwekwe nyeupe kwa kuwa zinamuonekano mzuri na ni rahisi kwa wachezaji kuona lango tofauti na nyavu nyekundu ambazo zinaendana na rangi ya jezi zao.

Mabosi wake hawakupinga pendekezo hilo kwa kuwa yeye ndiye bosi wa benchi la ufundi nandiyo maana ukichunguza sasa, nyavu za Anfield ni nyekundu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV