September 7, 2016

NDUSHA WAKATI AKISAJILIWA...

Wachezaji wawili wa Simba, Mousa Ndusha na Besala Bukungu ambao wote ni raia wa DR Congo, wametoa kauli ya kukata tamaa baada ya kushindwa kuitumikia timu yao hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu Bara zinazoendelea.

Wakongo hao ambao wamesajiliwa hivi karibuni, bado hawajapata hati zao za uhamisho wa kimataifa (ITC), hivyo hawaruhusiwi kucheza mpaka pale watakapokamilisha mchakato huo.

Ndusha amesema, wanaumizwa na hali hiyo inayoendelea kwa sasa lakini hawana cha kufanya huku wakilitupia lawama Shirikisho la Soka la DR Congo (Fecofa).

“Kiukweli inaumiza, sisi tumekuja kucheza soka Tanzania lakini inashangaza mpaka sasa hatuchezi si kwamba hatuna viwango, eti kwa kukosa ITC kitu ambacho kilitakiwa kupatikana mapema.


“Sasa hatuna jinsi inatubidi tutulie na kusubiri mpaka hapo tutakapozipata (ITC) ndiyo tuanze kucheza, kiukweli shirikisho letu kama halipo makini, ningeomba tu watufanyie haraka ili tuendelee kutafuta maisha ya soka huku,” alisema Ndusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV