September 14, 2016

Wakati Simba ikiendelea kufurahia mafanikio ya mechi zake nne za awali, imebainika kuwa straika wao tegemeo, Mrundi, Laudit Mavugo, amekuwa na rekodi ya ajabu kwamba kila anapofunga bao kwenye lango la Kaskazini basi timu hiyo haiongezi tena bao jingine na wala wapinzani hawataambulia kitu baada ya hapo.

Hiyo imethibitika katika mechi sita alizoichezea timu hiyo mpaka sasa tangu atue klabuni hapo akitokea Vital’O ya Burundi.

 Mechi mbili zikiwa za kirafiki na nne za michuano ya Ligi Kuu Bara.

Walipoumana na AFC Leorpads ya Kenya katika mchezo wa kirafiki huku ukiwa ndiyo mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya Simba, Mavugo alifunga bao kwenye dakika ya 81 katika lango la Kaskazini walipoibuka na ushindi wa mabao 4-0, hilo likawa bao la mwisho siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya Ndanda, Mavugo alifunga bao la kuongoza dakika ya 19 kwenye lango la Kusini, siku hiyo wapinzani wao walichomoa bao hilo kabla ya baadaye Fredric Blagnon na Shiza Kichuya kuifungia Simba bao moja kila mmoja na mechi ikaisha 3-1.



Katika michezo miwili iliyofuata, walipocheza na Ruvu, akafunga bao la pili katika lango la Kaskazini, hilo nalo likawa bao la mwisho siku hiyo na mechi ikaisha kwa matokeo ya 2-1.




Wikiendi iliyopita pia walipocheza na Mtibwa Sugar, Mavugo alifunga tena bao la pili kwenye lango la Kaskazini la Uwanja wa Uhuru na kama kawaida hilo likawa bao la mwisho kwa siku hiyo. Mchezo ukaisha Simba ikishinda 2-0.

Mbali na rekodi hiyo, lakini siku ikitokea pia Mavugo hakufunga bao basi hakuna timu itakayotikisa nyavu za mwenzake. Mchezaji huyo alipocheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya URA, mechi hiyo iliisha 0-0. Katika mchezo wao wa pili wa ligi waliocheza na JKT Ruvu, Mavugo hakufunga na matokeo yakawa 0-0.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic