September 14, 2016

Beki wa kulia wa Simba, Mkongomani Janvier Besala Bokungu, amesema kuwa yupo tayari kubadilishiwa nafasi kutoka beki wa pembeni na kucheza kama beki wa kati, kwani ndiyo nafasi aliyoicheza mara kadhaa kwenye kikosi cha TP Mazembe ya huko kwao.

Bokungu

Bokungu ambaye wikiendi iliyopita aliichezea Simba kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kupata hati yake ya uhamisho (ITC), alisema licha ya kumudu pembeni pia ni hatari akisimama kati, nafasi zinazokaliwa na Method Mwanjale, Juuko Murshid, Emmanuel Semwanza na Novaty Lufunga. 

Kauli hiyo ilikuja baada ya kuulizwa kuhusu changamoto ya namba katika nafasi yake ya beki wa kulia kutokana na uwepo wa Hamad Juma na Malika Ndeule ambao wanaonekana kufanya vema.

“Kweli changamoto ni kubwa, lakini bahati nzuri nina uwezo wa kucheza zaidi ya nafasi moja. Ninaweza kucheza kama winga pamoja na beki wa kati nafasi ambayo nimecheza mara kadhaa katika klabu nilizocheza huko kwetu (DR Congo) ikiwemo TP Mazembe,” alisema beki huyo.

Kiungo Mousa Ndusha yeye bado ITC yake mpaka jana Jumanne ilikuwa haijafika, hivyo kuishia kufanya mazoezi kikosini hapo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV