September 25, 2016


Las Palmas ikiwa nyumbani, imeilazimisha Real Madrid sare ya mabao 2-2 katika mechi ya sita ya La Liga.

Madrid ambayo ililazimika kumtoa Cristiano Ronaldo, ilishindwa kulinda bao moja ililokuwa inaongoza wakati La Palmas ikiwa ina bao moja na yenyewe mawili.

Marco Asensio alianza kuifungia MAdrid bao katika dakika ya 33 lakini Tana akaisawazisia Las Palmas kutoka katika visiwa vya Canaries ambavyo ni mali ya Hispania licha ya kuwa viko karibu kabisa na Morocco barani Afrika.


Dakika ya 67, Karim Benzema akaifungia Madrid bao la pili lakini juhudi binafsi za Ezequiel Arujo zikaisaidia Las Palmas kupata bao pili katika dakika ya 85 ikiwa ni dakika mbili tu tokea Ronaldo aende nje.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV