September 12, 2016

Klabu ya Manchester United imetangaza kuwa imeingiza mapato ya pauni milioni 515.3 katika msimu wa mwaka mmoja uliopita uliomalizika Juni 30, 2016.

Kutokana na kiwango hicho, klabu hiyo imesema kuwa imepata faida ya pauni 68 na kuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kuingiza pato la zaidi ya pauni nusu pauni ndani ya mwaka moja na pia imekuwa ya pili kwa kuingiza fedha nyingi nyuma ya Barcelona ya Hispania kwa ujumla.
 

 
Barcelona yenyewe itangaza kuingiza fedha pauni milioni 570 katika muda huohuo.

Licha ya kushindwa kufuzu kucheza katika Uefa Champions League, bado klabu hiyo imeendelea kuingiza mapato mengi kupitia malipo ya wadhamini yakiwemo yale ya runinga.





Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward amesema kuwa: "Kuteuliwa kwa Jose Mourinho ni moja ya njia zetu za kutufanya kuwa bora na kurejea kwenye ubora wetu, tupo katika mchamkato wa kuandika ukurasa mpya wa historia ya soka.”

Pamoja na hivyo, United ambayo ipo katika mkataba wa pauni milioni 750 ndani ya miaka 10 na kampuni ya adidas katika masuala ya jezi inatajwa kuwa na deni la pauni milioni 260.9.

Takwimu zinaonyesha kumfukuza kazi Louis van Gaal na wasaidizi wake kulisababisha klabu hiyo kupoteza pauni milioni 8.4 kama fidia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic