September 12, 2016

Straika mtata, Mario Balotelli ameanza vizuri katika timu yake mpya ya Nice kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Marseille katika Ligi Kuu ya Ufaransa, jana usiku.

Balotelli alitua klabuni hapo akitokea Liverpool baada ya kutohitajiwa na Kocha Jurgen Klopp.

Mchezaji huyo alishindwa kuwa na maisha mazuri ndani ya Liverpool ambapo pi alilazimika kutolewa kwa mkopo katika timu ya AC Milan lakini aliporejea Liverpool, Klopp akamwambia “hauna nafasi katika kikosi changu, we ondoka tu.”

  Katika mchezo wa jana, Balotelli alifunga bao la kwanza kwa njia ya penalti kisha bao la pili akaunganisha mpira wa krosi, ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu aanze kuichezea Nice.

Mara baada ya mchezo huo, Balotelli aliponda uamuzo wake wa kujiunga na Liverpool na kudai kuwa alifanya kosa kubwa kujiunga na timu hiyo.

“Ulikuwa ni uamuzi mbaya kuwahi kufanya katika maisha yangu, tofauti na mashabiki ambao walikuwa pamoja na mimi niwe mkweli sikuwa na uhusiano mzuri na wachezaji na kocha na sikuipenda klabu kwa jumla.


“Nilikuwa na makocha wawili, Brendan Rodgers na Jurgen Klopp, hawakuwa na msukumo kwangu na sikuwa nao karibu,” alisema Balotelli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV