September 2, 2016


Kiungo mpya wa Azam FC, Daniel Amoah, ameungana na wenzake na kuanza mazoezi kwenye viwanja vya Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Amoah raia wa Ghana aliyekuwa akiitumikia Medeama ya Ghana, ameonekana ni mwenye furaha chini ya makocha Wahispania wakiongozwa na Zeben Hernandez.

Raia huyo wa Ghana, ni kati ya viungo walioipa Yanga wakati mgumu wakati ikivaa Medeama katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV