September 13, 2016


Na Saleh Ally, Madrid
Nyota Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa nahodha wa kikosi cha Real Madrid.

Ronaldo anachukua nafasi hiyo rasmi na kuwa mmoja wa manahodha wane wa kikosi hicho.

Anachukua nafasi ya Alvaro Arbeloa aliyejiunga na West Ham United ya England. Sasa anaungana na manahodha wengine watatu ambao ni Sergio Ramos, Pepe na Marcelo.

Uamuzi wa Madrid kumpa unahodha mshambuliaji huyo inaonekana ni sehemu ya motisha kutokana na kufanya vizuri lakini ni kumfanya ajione hajapitwa na mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ambaye pia ni kati ya manahodha wane wa Barca.


Kumekuwa na mjadala mkubwa katakana na Ronaldo kuwa nahodha wa Los Blanco, wengine wakiamini imekuwa haraka sana na wengine wakiamini ni sahihi kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV