September 15, 2016

Kufuatia kuanza kuibuka kwa maneno mengi juu ya uwezo wa kiungo mpya wa Manchester United, Pau Pogba, ushauri umepelekwa kwa kocha wa timu hiyo jinsi ya kumfanya pogba awe mchezaji mwenye kiwango cha juu.

Kiungo wa zamani wa timu hiyo, Paul Scholes ndiye ambaye ametoa ushauri kwa Kocha Jose Mourinho akiwambia kuwa kama anataka Pogba awe mchezaji mwenye kiwango cha juu basi ana budi kumpanga pamoja na Michael Carrick.


Pogba amekuwa akipangwa pamoja na Marouane Fellaini katika safu ya kiungo lakini alishindwa kuwika katika mchezo wa Manchester derby, Jumamosi iliyopita.

"Siyo mzuri sana kwenye kuuchezea mpira, unatakiwa kukumbuka kuwa ametua United akitokea kwenye kikosi kizuri cha Juventus. Huko alikuwa na kina Andrea Pirlo na Claudio Marchisio ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na kumpa nafasi ya kucheza.

"Ningependa kumuona Michael Carrick akicheza naye pale katikati, anaweza kumpa mwangaza wa wapi pa kuelekea,” alisema Scholes.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV