September 15, 2016

Kocha Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte amesisitiza kuwa kiungo, Cesc Fabregas ni mtu muhimu na bado yumo kwenye mipango yake msimu huu, licha ya kutomtumia katika mechi nne za mwanzo za Ligi Kuu England mpaka sasa.
Fununu zilizopo juu ya majaaliwa ya Mhispania huyo ni kwamba huenda akapisha njia kikosini hapo kutokana na kocha huyo kuwatumia zaidi Oscar sambamba na Nemanja Matic na N'Golo Kante aliyetua msimu huu.


Hata hivyo alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumuuza Fabregas kwenye dirisha dogo la usajili, Januari, Conte alijibu: "Hapana, hapana, hapana. Cesc bado yumo kwenye mipango yangu na mimipango ya Chelsea pia. 


Sote tunajua Cesc ni mchezaji hatari. Katika kila mazoezi, namuona ni mtu mwenye ari kubwa. Kama akiendelea namna hii, nitakuwa na wakati mgumu kuchagua kiungo wa kumtumia.

"Hiki ndicho ninachokitaka kwa mchezaji, niwe na hofu ya nani nimchague kucheza. Cesc  ni mchezaji mkubwa, kila mmoja anamjua. Na sasa naanza kumuelewa kama mwanaume wa kazi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV