September 15, 2016


Kiungo wa zamani wa Chelsea, Michael Essien, anajiandaa kujiunga na timu ya Australia, Melbourne Victory.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea kwa sasa anakitumikia kikosi cha Panathinaikos cha nchini Ugiriki ambacho alijiunga nacho akitokea AC Milan mwaka 2015.

Amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na klabu hiyo lakini inaelezwa anaweza kuondoka na kujiunga na klabu hiyo ambayo itakuwa ya nane kwenye maisha yake ya soka.
Kwa mujibu wa gazeti la nchini Australia Herald Sun, Essien, 33, anatarajiwa kufanya mazungumzo ya mwisho na kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV