September 15, 2016

Mchezaji mahiri wa zamani wa West Ham na Lazio, Paolo Di Canio ametimuliwa kama mchambuzi wa kituo cha televisheni cha Sky Sport Italia.

Kocha huyo pia wa zamani wa Swindon na Sunderland, amekuwa akifanya kazi hiyo ya uchambuzi kwenye televisheni hiyo kitengo cha Italia kwa muda mrefu.
 






Enzi zake alipokuwa akicheza

Hata hivyo, kocha huyo alitimuliwa juzi baada ya kuonyesha tattoo iliyopo kwenye mwili wake ambayo inaunga mkono kundi la kifashiti la Dux ambalo lipo chini ya kiongozi Benito Mussolini.

Di Canio, mara nyingi amekuwa akichambua soka kwenye televisheni hiyo akiwa amevaa suti lakini juzi alivaa tisheti ambayo ilisababisha tattoo hiyo ikaonekana.

Mara kadhaa mchezaji huyo amekuwa akikumbwa na adhabu kutokana na kuonyesha imani yake chini ya makundi hayo ya kifashiti kwani mwaka 2005 aliwahi kufungiwa mchezo mmoja wakati akiwa kwenye Ligi ya Serie A, baada ya kushangilia kwa kutumia staili ya kundi hilo.

 Inaelezwa kuwa baada ya tattoo hiyo kuonekana wachambuzi mbalimbali na na watu kwenye mitandao ya kijamii walianza kulalamikia hali hiyo ndipo Sky wakaamua kumtimua.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic