September 3, 2016Hayawi hayawi, Shamsa Ford aolewa
STAA wa Bongo filamu nchini, Shamsa Ford jana amefunga ndoa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo.

Sherehe za ndoa hiyo zimefanyika nyumbani kwa wazazi wa Shamsa eneo la Sinza, Afrikasana jijini Dar es Salaam jana.

Awali, Shamsa alidumu katika penzi na Dickson Matoke ‘Dick’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry na kisha kufunga ndoa ya kimila nyumbani kwa mwanaume huyo, Tarime mkoani Mara ila baadaye waliachana na kuangukia kwa staa wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambaye penzi lao halikudumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV