October 13, 2016


Baada ya kuziona nyavu kwa kuifungia Yanga bao, Obey Chirwa amesema anaamini ataendelea kufanya vizuri.

Chirwa raia wa Zambia amekuwa katika wakati mgumu hadi alipofunga bao wakati Yanga ikiivaa Mtibwa Sugar na kuitwanga kwa mabao 3-1.

“Najua tunavyoshirikiana, tunavyofanya kazi yetu kwa pamoja kwa lengo la kuisaidia timu. Natamani kufunga, pia natamani kutoa pasi za mabao. Nitasaidiana na wenzangu na kufanya vizuri,” alisema Chirwa.

Mshambuliaji huyo alifunga bao safi la shuti kali, likiwa la kwanza kwake kwenye ligi na alikimbia kwenda kumkumbatia kocha wake, Hans van der Pluijm.


Pamoja na Chirwa kuonekana ni mchezaji mzuri, suala la presha limeonekana kumpa wakati mgumu na kufunga bao, huenda kukamsaidia kufanya vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV