October 18, 2016


Nahodha wa Yanga, Nadir Ali Haroub maarufu kama Cannavaro amesema bado siku chache itarejea katika fomu yake na kurejea kileleni.

Cannavaro amesema Yanga inapita katika kipindi kigumu na kitakuwa cha muda.

“Kweli sasa inaonekana ni kipindi kigumu kwa Yanga, lakini hili suala litapita na ninakuhakikishia Yanga itarudi katika hali yake,” alisema.

Yanga iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi nane za Ligi Kuu Bara.


Inaonekana mwendo wa Yanga si ule ambao umekuwa wa misimu miwili iliyopita, huku watani wao Simba wakiwa na kasi kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV