HAJI Manara, usajili mpya ndani ya Yanga katika kitengo cha habari ameweka wazi kuwa yeye hana kisasi ila ana nongwa ya kahawa huku akigusia dili la mzigo wa bilioni 20 za Simba.
Manara alitambulishwa ndani ya Yanga, Agosti 24 mbele ya Waandishi wa Habari na kukabidhiwa jezi ya Yanga na kazi yake ya kwanza ilikuwa ni Agosti 25, Mlimani City ambapo alitambulisha jezi mpya za Yanga.
Akiwa ndani ya Simba aliweza kudumu kwa muda wa miaka sita alikuwa ni Mkuu wa Kitengo cha Habari alisepa ndani ya kikosi hicho baada ya kuwaaga mabosi wake kupitia kundi la Simba HQ na taarifa rasmi ya kusepa kwake Simba ilitolewa Agosti 28.
Manara amesema:"Mimi kisasi sina ila nina nongwa ya kahawa. Kahawa kikombe chake kidogo kinaunguza, hiyo ni sifa yake mbaya, pili ya moto, tatu siku hizi wanaongeza pilipili mtama, tangawizi , sijui mavitu gani hii ni sifa mbaya nina nongwa ya kizaramo haiishi.
"Sitawafanyia nongwa Simba, siwezi kama wenyewe wanavyojinasibu kuwa Simba ni kubwa kuliko mtu yoyote. Mimi nina nongwa kwa sababu nilitumia nguvu kubwa kuibrand timu ile na kuwaaminisha watu yasiyowezekana na mengine yaliwezekana.
"Kwa mfano baada ya sakata lile siku tatu mbele ikatengenezwa press, (Mkutano) kunitoa njiani mimi ikatengenezwa press na bango kubwa likawekwa. Tusiongopeane ile ni taasisi kubwa, unasema umeweka bilioni 20, benki gani?
Katika mkutano huo unaozunguziwa ni cheki ya bilioni 20 ambayo ilisainiwa ikiwa ni sehemu ya uwekezaji ndani ya kikosi hicho.
Na huku Simba ikizidi kushamiri
ReplyDeleteManara bado ni msemaji wa simba bila ya yeye mwenyewe kujitambua. Anaizungumzia sana simba kuliko ajira yake mpya. Ni ngumu sana kuiacha asili
ReplyDeleteHiyu nae atumie hata qkili kidogo iliyobaki basi, aachane na kelele za simba wenyewe wamesha muignore. Ahangaike na ajira yake mpya
ReplyDeleteUtopolo hakuna jipya la kuzungumzia ndiyo maana kila kukicha anazungumzia Simba.... Na asipo angalia huko aliko sasa hatapata kitu positive cha kuzungumzia matokeo yake kila siku atakuwa anatafuta maneno ya kuichafua simba
DeleteSio kuwa wanampuuzia, wanajua wakijibu atasema makubwa zaidi. Wanaomba apoe..Hahaha
ReplyDeletePole sana
DeleteAtulie si ameshaajiriwa na aliokuwa anawapelekea siri za Simba? Pesa na mambo ya Simba hayamhusu
ReplyDeleteHawana haja ya kubishana na mtu anayetapatapa asije akawarushia tope, bora walivyompuuza.
ReplyDeleteKukaa kimya pia ni hekima kubwa.
ReplyDeleteKukaa kimya ni hekima kubwa pia na haimaanishi wanamuogopa
ReplyDeleteAsijibiwe akijibiwa ndio kaokolewa
ReplyDeleteMimi ninamshauri Bw. Mdogo Manara aachane na habari za Simba. Yeye kwa sasa ahangaike na kazi ya kuibrand timu yake Yanga ili angalao iikaribie karibie Simba
ReplyDelete